A
- Adhabu ya kaburi ajua maiti.
- Adui mpende.
- Afua ni mbili, kufa na kupona.
- Ahadi ni deni.
- Akili mali.
- Akomelepo mwenyeji na mgeni koma papo.
- Akutendae mtende, simche akutendae.
- Aliye juu yu juu: mbwidi haliwi ni funo.
- Aliye k’ando haangukiwi ni mti.
- Aliyepeka mkono kutamalaki si kazi.
- Amani haiji illa kwa n’ta ya upanga.
- Ametoa nguo jogoi, mkewe hakuzipata.
- Angenda juu kip’ungu hafikilii mbinguni.
- Asiye nathari, sandamani nae.
- Asiyekuridhi mridhi.
- Asiyenitua kwa hili langu, akiwa na lakwe nasitumai.
- Asiyeona kwa yeye na akionywa haoni.
- Asojua kufa, nangalie ng’ombe.
- Asoweza kutuumba kutuumbua hawezi.
- Auguwae huangaliwa.
B
- Baada ya dhiki faraji.
- Bamba na waume bamba; hakuna bamba la mume.
- Bandu, bandu,—humala gogo.
- Bora afia.
- Boriti ina mwandamizi wakwe.
C
- Cha kitwa ki tamu na cha mkia ki tamu.
- Chanda chema huvikwa p’ete.
- Chanda na p’ete, ulimi na mate, uta na upote.
- Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
- Chema hakikai, hakina maisha.
- Chua mzuia-maji ndovu akitamani.
D
- Dalili ya mvua ni mawingu.
- Dunia huleta vyema na vimbi.
- Dunia k’itu dhaifu: kiumbe sijietee.
- Dunia mti mkavu: kiumbe siulemele.
- Dunia mwendo wa ngisi, kamwe msililiwale.
- Dunia ni mduwara: huzunguka kama p’ia.
- Dunia si k’itu, sijetee nayo.
F
H
- Haba na haba hujaza kibaba.
- Habari ina kishindo.
- Habari ya uwongo ina n’ta sabaa: habari ya kweli ina n’ta moja.
- Haina tabibu ndwee ya mapendi.
- Hakuna kubwa lisiloshindwa.
- Hakuna msiba usio mwenziwe.
- Hakuna refu lisilo n’ta.
- Hakuna zaidi mbovu: Fungat’o haiumizi mkono.
- Halipati! halipati!—lapumbaza.
- Hamadi ni iliyo bindoni: silaha ni iliyo mkononi.
- Hamna! hamna!—ndimo mliwamo.
- Haongezwi muongezi.
- Haraka haraka haina baraka
- Haurambwa mkono mtupu.
- Hawi Musa kwa kutukua fimbo.
- Heri adui mwerevu kama rafiki mpumbavu.
- Heri kenda, Shika! kama kumi, Enda uje!
- Heri kukuwaa kidole kama kukuwaa ulimi.
- Hishima ya kiungwana, hujua atendewayo.
- Hivi sasa ni muovu: hifa utanikumbuka.
- Howe! nda mwenyi kufuma: wewe una Howe! gani?
- Humpendaje mt’u kwa kwambiwa Penda.
- Hutafutaje jambia na mtoto hajazawa?
- Hutendwaje ikafana, subili ikawa tamu?
- Huwaje kuisaliti nyama ndavu na asali?
I
- Iizayo ndiyo ipendayo.
- Ilimu ndiyo muanga yongozayo kulla shani.
- Imara ya jembe kaingoje shamba.
- Ivushayo ni mbovu.
J
- Jawabu na wakatiwe, na wakatiwe si zani.
- Jitihadi haiondoi amri ya Mngu.
- Jivuli la mvumo humfinika aliye mbali.
- Jungu bovu limekuwa magae.
- Juzi na jana si kama ya leo.
K
- K’anga hazai ujani.
- K’avu haisuki, siuze koroma.
- K’itu ni futa la moyo: humpa umpendae.
- Kasikazi mja na-swi, Kusi mja na mtama.
- Kawaida ni kama sharia.
- Kazi isiyo faida kutenda si ada.
- Kazi isiyo kipimo mwishowe wat’u huteta.
- Kazi yangu ifanyet’o, usifanye kwa kinyongo.
- Kazi-mbi, si mtezo mwema.
- Kenda karibu na kumi.
- Kidole kimoja hakivundi t’awa.
- Kifo ki karibu: ki kishogoni mwako.
- Kigumba kwa ngue, kwa mlimwengu ki utungu.
- Kijana ukimnyang’anya kisu mpe kijiti.
- Kikulacho ki nguoni mwako.
- Kilemba ni shiba ya nguo.
- Kilicho baharini kalingoje ufuoni.
- Kilichoniuma jana ‖ Utunguwe hauona ‖ Hakinitambai tena.
- Kilimia kikizama kwa jua huzuka kwa mvua, kikizama kwa mvua huzuka kwa jua.
- Kimya kingi kina mshindo mkuu.
- Kinga na kinga, ndipo moto uwakapo.
- Kionda-ndugu chapoa?
- Kipaka kidogo hakipigiki na-t’i.
- Kipya ki nyemi, kingawa kionda.
- Kisauni kutamea mvinde?
- Kitema k’uni temat’o.
- Kukimbia si kufika