Lugha

Kigiryama

Methali 35 za Kigiryama, kila moja na maana yake, mfano wa matumizi na rejeo la chanzo.

35 methali

Methali za Kigiryama

Kigiryama · Ukarimu

Mwenda-kwao k'afungwa m'lala.

Kiswahili Anayerudi kwao hafungwi ukanda wa mlala.

Mgeni anayeondoka hapaswi kubebeshwa mizigo ya kazi na ujumbe usiomhusu.

Kigiryama · Mipango

Mwenda-mbere k'aheka madzi vundzu.

Kiswahili Anayetangulia kufika hachoti maji machafu.

Anayewahi hupata kilicho bora kabla wengine hawajakiharibu.

Kigiryama · Maneno

Nambira kiré nyumba kiré mvungu kisikire.

Kiswahili Namwambia mtoto aliye ndani ya nyumba, ili yule aliye mvunguni asikie.

Mara nyingine mtu huelekeza maneno kwa mwingine ili yamfikie mtu wa tatu anayesikiliza.

Kigiryama · Mali

Nyumba ya p'ombe k'aikala p'ombe.

Kiswahili Katika nyumba ya pombe, pombe haikai.

Ulevi humaliza mali, na nyumba yenye ulevi haibaki na akiba.

Kigiryama · Mali

T'embe na t'embe ni mukahe.

Kiswahili Punje na punje huwa mkate.

Vitu vidogo vikikusanywa kidogo kidogo huwa kitu kikubwa chenye manufaa.

Kigiryama · Mali

Tama si kit'u, kidzo ni m'vera.

Kiswahili Matumaini si kitu; kizuri ni kile ulicho nacho mkononi.

Kilicho mkononi au kuridhika na ulicho nacho ni bora kuliko kutegemea matumaini matupu.

Kigiryama · Tahadhari

Tama yarya m'tsumi.

Kiswahili Tamaa ilimla mtafuta faida.

Tamaa ya faida inaweza kumpeleka mtu kwenye hatari inayomwangamiza.

Kigiryama · Urafiki

Ts'i na mahako k'avitsowana.

Kiswahili Kiti na mkalia havitengani kamwe.

Vitu au watu wanaotegemeana daima huwa pamoja na hawatengani.

Kigiryama · Mali

Udzichorya ndo chako.

Kiswahili Ulichokula ndicho chako.

Mali ya dunia haina uhakika; kilicho chako kweli ni kile ulichokwisha kukitumia.

Kigiryama · Tahadhari

Vuri ni kitima-ngilo.

Kiswahili Mvua za vuli ni panzi arukaye mbali.

Kisichokuwa na uhakika hufika hapa na kukosa pale, hivyo usikitegemee kikamilifu.

Unajua methali ambayo bado haipo hapa?

Tuma methali, chanzo au marekebisho. Wahariri hukagua kila mchango kabla ya kuuchapisha.

Changia methali

Bila kujisajili