Methali ya Kiswahili

Kuonana k’olewa.

Maana kwa kifupi

Kukutana kwa marafiki kumepangwa na Mungu, si kwa bahati tu.

Ufafanuzi wa methali

Taylor anaeleza kuwa k'olewa ni ni kuolewa, kutoka kwenye mzizi wa zamani wenye maana ya kunyoosha, kuelekeza na kuamuru. Anasisitiza kwamba katika Kiswahili cha zamani mzizi huu ni tofauti na kuoa kwa maana ya ndoa. Kwa maelezo yake, rafiki wawili wakiagana humkumbusha mmoja mwingine kwamba hawakukutana kwa bahati.

Hutumiwa lini?

Unapoagana na rafiki baada ya kukutana kwa namna iliyowaletea manufaa au furaha.

Mfano wa matumizi

Tumaini na rafiki yake wa utotoni walikutana ghafla stendi ya Arusha, wakazungumza kwa saa nzima. Walipoagana, kila mmoja alimshukuru Mungu kwa siku hiyo.

Unajua methali ambayo bado haipo hapa?

Tuma methali, chanzo au marekebisho. Wahariri hukagua kila mchango kabla ya kuuchapisha.

Changia methali

Bila kujisajili